Mlima Everest:Mlima wa Choo

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mamilioni ya wakwea mlima Everest ambao ndio mlima mrefu duniani huwacha uchafu na kinyesi cha binadamu katika eneo hilo

Uchafu mwingi pamoja na kinyesi cha binaadamu huwachwa katika mlima wa Everest ambao ndio mlima mrefu duniani.

Takataka hizo huchafua mazingira na zinaweza kusababisha magonjwa, kulingana na mkuu wa muungano wa wakwea mlima huko Nepal.

Ang Tshering anaitaka serikali ya Nepal kuwaagiza wakwea mlima kuondoa uchafu wao.

Image caption Wakwea mlima katika mlima Everest

Anasema kuwa uchafu huo umerundikana kwa miaka kadhaa sasa.

''Wakwea mlima huchimba mashimo katika barafu na kufanya haja kubwa ''.

Zaidi ya wakwea milima 700 pamoja na viongozi wao hukaa kwa miezi kadhaa katika mteremko wa mlima huo kila mwaka.

Image caption Uchafu uliopo katika mlima Everest

Kuna msimu wa kukwea mlima Everest ambao huanza wiki hii na kukamilika mwezi May.

Wakati mwengine wa mwaka hali ya hewa huwa mbaya.

''Ni hatari ya kiafya na tatizo hilo linafaa kujadiliwa'',alisema Dawa Steven Sherpa,ambaye amekuwa akisaidia kuusafisha mlima huo tangu mwaka 2008.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kilele cha mlima Everest

Anasema kwamba baadhi ya wakwea mlima hutumia mifuko ya plastiki kufanya haja zao wakati wanapoishi katika kambi zilizopo katika mlima.

Katika kambi zilizopo chini ya mlima kuna vyoo vya mahema, ambavyo vina mapipa maalum ya kuhifadhi uchafu wa kinyesi.

Mapipa hayo yanaweza kusafirishwa kutoka mlima huo na kumwaywa.