Wamshtaki Mugabe kwa kuwafuta kazi

Image caption Mugabe ashtakiwa kwa kuwafuta kazi kiholela rafikize

Washirika wawili wa zamani wa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe wanamshtaki kwa kuwafuta kazi kiholela.

Rigare Gumbo ambaye alikuwa msemaji wa chama tawala cha ZANU-PF na Didymus Mutasa ,katibu mkuu wa chama hicho walifutwa kazi mwezi Disemba na Februari.

Walishtumiwa kwa kujaribu kumsaidia aliyekuwa makamu wa rais Joice Mujuru kumpindua rais Mugabe.

Waandishi wanasema kuwa mashtaka yao dhidi ya kiongozi huyo wa miaka 91 sio ya kawaida.