Kikwete akutana na viongozi wa albino

Image caption Wenye ulemavu wa ngozi na walemavu wengine wakiwa Ikulu ya Tanzania

Baadhi ya walemavu wa ngozi yaani albino mapema Alhamisi walifanya vurugu nje ya Ikulu ya Tanzania wakati viongozi wao wakisubiri kuingia katika kikao na Rais Jakaya Kikwete.

Rais Kikwete alikuwa akitarajiwa kufanya mkutano na viongozi wa Albino Tanzania TAS, aliowaalika kuzungumzia hoja zao kutokana na mauaji ya walemavu hao yanayoendelea nchini humo.

Kutokana na vurugu hizo maafisa wa Ikulu waliwatawanya walemavu hao kutoka nje ya geti.

SAHIHISHO

Hatimaye Rais Kikwete aliweza kukutana na viongozi hao baada ya mtafaruku kudhibitiwa. Tunaomba radhi kwa usumbufu uliotokea kutokana na taarifa ya awali kuwa kikao hicho kiliahirishwa.