Kinara wa Nusra adaiwa kuuawa syria

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanamgambo wa Nusra front wenye uhusiano na Al Qaeda

Vyombo vya habari vya Serikali ya Syria vimesema jeshi limemuua kamanda wa kijeshi kutoka kundi la waasi lenye uhusiano na Al Qaeda, la Nusra Front.

Taarifa zinasema aliuawa katika mji wa Idlib ambapo viongozi wa Nusra Front walikuwa wanakutana.

Nusra front ni moja kati ya makundi yenye nguvu yanayopambana ili kumuangusha Rais wa Syria, Bashar Al Assad, kundi hilo pia lilihusika na shambulizimjini Aleppo siku ya jumatano.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Syria ameweka wazi nia yake ya kufanya mazungumzo na Nusra Front ikiwa sehemu ya jitihada za kurejesha utulivu mjini Aleppo.

Staffan de Mistura ameiambia BBC kuwa yuko tayari kufanya mazungumzo na yeote ili kuokoa maisha ya Watu mjini humo.