Tamko la Facebook lamtia mashakani

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Tamko la facebook limtia mashakani raia wa marekani anayefanya kazi katika milki za kiarabu

Raia mmoja wa Marekani anayefanya kazi katika mataifa ya milki za kiarabu UAE amekamatwa kwa matamshi aliyochapisha katika mtandao wake wa facebook, na sasa anakabiliwa na hukumu ya kufungwa jela.

Ryan Pate,ambaye ni fundi wa ndege alikuwa katika likizo ya kujiuguza nyumbani kwake katika jimbo la Florida nchini Marekani wakati alipomkosoa mwajiri wake.

Aliita kampuni hiyo kama yenye ''wasaliti na kutoa matamshi ya kibaguzi dhidi ya watu wa mataifa ya milki hiyo.

Wakati alipokuwa akirudi alikamatwa kwa kukiuka sheria kali za taifa hilo kuhusu matamshi ya kashfa .

Iwapo atapatikana na hatia huenda akahudumia kifungo cha hadi miaka mitano jela.