Zaidi ya Watu 60 wapoteza maisha Nigeria

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wakazi wamekuwa wakiyakimbia makazi yao kutokana na mashambulizi ya Boko Haram

Zaidi ya Watu 60 wameuawa na kundi la watu wanaodhaniwa kuwa Boko Haama kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Wakazi wa wanasema Wanamgambo wa kiislamu walishambulia kijiji cha Njaba katika jimbo la Borno alfajiri ya jumanne, na kuwaua Watu wakiwemo vijana wadogo.

Shuhuda mmoja katika kijiji hicho ameiambia BBC kuwa watu walilazimika kuyakimbia makazi yao na kuwaacha waliopoteza maisha, wamekuwa wakihofu kurejea.