Islamic state yaharibu mji wa Nimrud

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Iraq yadai wapiganaji wa IS wanaendelea kuharibu mji wa kihistoria wa Nimrud Iraq.

Maafisa nchini Iraq wanasema kuwa wapiganaji wa Islamic State wanaendelea kuharibu mji wa Nimrud - moja ya sehemu yenye vito wa thamani inayoheshimiwa katika historia ya Iraq.

Wizara ya utalii nchini Iraq imesema wapiganaji hao wanatumia vifaa vikubwa kuharibu eneo hilo.

Tukio hilo limetajwa kuwa uharibifu wa utamaduni na jaribio la kuharibu Nimrud ambayo imelinganisha na uharibifu wa mwamba wa Taliban wa

Bamiyan buddha huko Afghanistan mwaka 2001.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Moja ya sanamu zenye historia kubwa ya taifa la Iraq

Kulingana na wizara ya turathi ya Iraque wapiganaji wa IS waliingia katika mji huo wa kale wakitumia matingatinga na silaha nyingine nzito na wakaharibu kituo hicho.

Nimrud ilipewa jina hilo baadaye na waarabu lakini awali ilikuwa inaitwa Kalhu,

Ambayo iliundwa katika karne ya kumi na tatu kabla kuzaliwa kwa Yesu Kristu na pia inaonekana katika agano la kale. Ni sehemu kubwa lakini haijulikani hasa ikiwa imeharibiwa yote.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Sanamu zikiharibiwa

Vinyago kutoka Nimrud – vinavyojumuisha sanamu za mafahali zilizochongwa kwa mawe ziko katika makavazi mengi kote duniani.

Mwezi uliopita, Islamic State walitoa kanda ya video inayoonyesha wapiganaji wakiharibu na kusaga saga vitu vya thamani katika makumbusho ya Mosul.

Kundi hilo la wapiganaji limesema vitu hivyo viko kinyume cha maadili ya dini ya kiislamu.