Ebola:Mgonjwa wa mwisho atolewa Liberia

Image caption Beatrice Yardolo

Mamlaka nchini Liberia inasema kuwa imemruhusu kwenda nyumbani mgonjwa wa mwisho wa Ebola na kuanza kuhesabu siku zilizosalia kwa taifa hilo kutangazwa lisilo na visa vyovyote vya Ebola.

Beatrice Yardolo mwenye umri wa miaka 58 ambaye alitolewa kutoka kituo kimoja cha matibabu ya ugonjwa wa ebola kinachosimamiwa na Uchina katika mji mkuu wa Monrovia ameiambia BBC kwamba yeye ni miongoni mwa watu walio na furaha chungu nzima duniani.

Liberia sasa imesalia na siku 42 kutangazwa kama taifa lisilo na visa vyovyote vya ugonjwa wa ebola kulingana na maelezo ya shirika la Afya duniani WHO.

Takriban raia 4000 wa Liberia wamepoteza maisha yao kutokana na ugonjwa huo.