Wadaiwa kushirikiana na Al-Shabaab

Haki miliki ya picha AP
Image caption wanajeshi wa ngazi za juu nchini Somalia wanachunguzwa kwa kushirikiana na kundi la wapiganaji wa Alshabaab

Mamlaka nchini Somalia imewakamata wanajeshi wake wa ngazi za juu na kuwatuhumu kwa kushirikiana na wapiganaji wa kundi la Al-shabaab.

Tayari maafisa 12 wanachunguzwa kwa madai ya kuwasaidia wapiganaji hao kushambulia hoteli ya The SYL katika mji mkuu wa Mogadishu mnamo mwezi Januari.

Ujumbe kutoka Uturuki ulikuwa ukiishi katika hoteli hiyo ukisubiri ziara ya rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption wanajeshi wa umoja wa Afrika nchini Somalia

Watu watatu waliuawa katika shambulizi hilo la bomu.

Jeshi la serikali ya Somali linalosaidiwa na vikosi vya Umoja wa Afrika linajaribu kulishinda kundi la Al-shabaab.