Mazungumzo Sudan Kusini yagonga mwamba

Image caption Viongozi wa Sudan Kusini

Mazungumzo ya kutatua mzozo unaokumba Sudan Kusini yamegonga mwamba, saa kadhaa kabla ya Umoja wa Mataifa kuwawekea makataa wanaohusika.

Rais wa nchi hiyo, Salva Kiir na mpinzani wake ambaye aliwahi kuwa makamu wake, Riek Machar, wamekuwa wakijadili mipango ya kugawanya mamlaka ili kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimesababisha maelfu ya watu kuuawa na zaidi ya watu milioni moja unusu kupoteza makao.

Umoja wa mataifa umetishia kuwawekea vikwazo watu binafasi wanaojaribu kuzuia makubaliano hayo iwapo makundi hayo mawili hayatatia saini mwafaka kabla ya muda uliotengwa.