Iraq yataka kuikomboa Tikrit

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Tikrit hali ilivyo

Kumekuwa na wasiwasi mkubwa kwa maelfu ya raia wa Iraq,wakati huu ambapo jeshi la serikali la nchi hiyo linaingia siku ya nne ya mapambano ya kutaka kuukomboa mji wa Tikirit.

Kufuatia hali hiyo, umoja wa mataifa umetuma misafara ya misaada kwa maelfu ya raia hao wanaoaminika kutawanyika kila upande wa nchi hiyo baada ya mji huo kushikiliwa na wanamgambo wa dola ya kiislam Islamic State .

Ikulu ya Marekani na shirika la kimataifa cha kutetea haki za binaadamu limeonya juu ya hatari ya ghasia ambazo zinaweza kusababishwa na madhehebu ya kidini yanayoungwa mkono na Iran hasa wanajeshi wa Ki Shia ambao wana husika kwa kiasi kikubwa katika ghasia hiyo.

Maelfu ya askri wa ki Shia waliuawa mwaka jana wakati wanamgambo wa dola ya kiislamu walipoutwaa mji wa Tikrit. Ghasia hizo zilizorota kutokana na mabomu ya barabarani na hata mitego iliyowekwa na wanajeshi.

Mwandishi wa BBC anasema kwamba serikali ya Iraq inataka kuuzunguka mji huo na kuukaribia mji wa Tikrit na vitongoji vya jirani kabla hawajauingia mji huo.