Mkanyagano watokea katika kivuko Kenya

Image caption Mkanyagano watokea katika kivuko cha likoni huko Mombasa Kenya

Ripoti zinasema kuwa mkanyagano umetokea katika kivukio cha Ferry katika eneo la Likoni huko Mombasa Kenya na kuwajeruhi watu kadhaa

Tukio hilo limejiri baada ya ferry tatu zinazoendesha oparesheni zake katika kivuko hicho kukabiliwa na matatizo ya kiufundi.

Kulingana na ripoti hizo Ferry zilizosalia zimeshindwa kuhudumia idadi kubwa ya watu wanaotumia kivuko hicho pamoja na ile ya magari.

Hatua hiyo imesababisha msongamano mkubwa wa watu katika kivuko hicho.