Dereva Mpalestina awagonga Waisraeli

Image caption Dereva wa kipalestina alivurumisha gari lake katikati ya kundi la raia wa Israel

Polisi nchini Israeli wanasema kuwa dereva ambaye anaaminiwa kuwa Mpalestina amevurumisha gari katikati ya kundi la watu kwenye mtaa mmoja mjini Jerusalem.

Wanasema kuwa mwamamume huyo aliwajeruhi takriban wapita njia wanne na kisha akajaribu kumchoma kisu mtu mwingine kabla ya kupigwa risasi na kujeruhiwa na maafisa wa usalama.

Msemaji wa polisi amekitaja kitendo hicho kuwa shambulizi la kigaidi.

Kulishuhudiwa visa vingine kama hivyo mwaka uliopita vilivyoendeshwa na madereva wa Kipalestina ambapo watu watatu waliuwa.