UN yawaagiza waasi kuweka amani Mali

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban ki Moon

Katibu mkuu wa umoja Ban ki Moon ametaka waasi wa Tuareg nchini Mali kutia sahihi makubaliano ya amani yenye lengo la kuleta utulivu eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.

Makubaliano hayo yaliyoafikiwa nchini Algeria tayari yamesainiwa na serikali ya Mali na makundi mengine sita yaliyojitenga.

Makubaliano hayo yanaruuhusu kuwepo mamlaka zaidi katika eneo la kaskazini mwa nchi.

Image caption Waasi wa kundi la Tuareg nchini Mali

Eneo kubwa kaskazini mwa Mali lilidhibitiwa na wanamgambo wa kiislamu mwaka 2012 lakini walitimuliwa na wanajeshi wa ufaransa mwaka uliofuatia.

Hata hivyo makundi mengine ya Tuareg bado yanaendesha harakati zao.