Polisi walaumiwa na familia za wasichana

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Familia za wasichana wa Uingereza waliotoroka na kuelekea Syria ili kujiunga na Islamic state

Jamaa za wasichana watatu raia wa Uingereza ambao walikimbia nyumbani na kujiunga na wanamgmbo wa Islamic State nchini Syria wamewashtumu vikali maafisa wa polisi kwa kushindwa kuwafahamisha moja kwa moja kabla kutoweka kwao.

Polisi walikuwa wamepanga kuwahoji wasichana hao kuhusu rafiki yao ambaye tayari alikuwa amesafiri kwenda nchini Syria ambapo waliwaandikia barua wazazi wao kuwaomba ruhusa.

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Wasichana watatu wa Uingereza waliotorokea nchini Syria

Badala ya kupeleka barua walizopewa na polisi nyumbani waliamua kuzificha.

Wachunguzi wanasisitiza kuwa hakuna dalili zilizoonyesha kuwa wasichana hao walikuwa na nia ya kusafiri kwenda nchini Syria.