Kampuni yawaomba msamaha wanawake

Haki miliki ya picha AFP
Image caption wanawake wakifanya maandamano kuadhimisha siku ya wanawake duniani nchini Indonesia

Kampuni inayotengeneza nguo za riadha nchini Indonesia, imeomba msamaha, kwa kuuza t-shati za kandanda, ambazo zina maelekezo kuhusu namna ya kuzifua.

Maelekezo ya kizungu, yanasema:"T-shati hii mpe mwanamke akufulie.Hiyo ni kazi yake."

Kampuni hiyo, Salvo Sports, imesema maelekezo hayo yamefahamika vibaya na kwamba hayakukusudia kumdharau mwanamke, ni kusema kuwa mwanamke ni mjuzi zaidi.

Jazi hiyo ilikusudiwa timu ya ligi ya Indonesia, Pusamania Borneo.