Rais Edgar Lungu kutibiwa nje ya Zambia

Image caption Raisi Edgar Lungu, wa Zambia

Raisi mteule wa Zambia Edgar Lungu ,ameshauriwa na madaktari kwenda kufanyiwa matibabu na wataalamu wa afya nje ya nchi yake ili afanyiwe marekebisho ya utumbo wa chakula ambao husinyaa na kumfanya aanguke mwishoni mwa juma lililopita.

Vipimo vilivyochukuliavya Raisi Lungu na kupelekwa katika hospitali ya kijeshi katika mji mkuu wan chi hiyo Lusaka,vimeonesha kwamba raisi huyo ana vimelea vya malaria .Raisi Lungu ana umri wa miaka 58,alipaswa kuacha shughuli ya kilele cha siku ya wanawake duniani katika mji mkuu wanchi hiyo siku ya Jumapili,pindi alipokuwa hajisikii vyema.

Ushauri wa madaktari kumtaka Raisi Lungu akatibiwe nje ya nchi yake, unatokana na kutokuwa na tiba ya hali ya juu ya kiteknolojia anayostahili kupata raisi huyo haipatikani nchini mwake,na hivyo inamlazimu kwenda ng’ambo kwa matibabu.

Lungu anatoka katika mji wenye kuongoza kwa uzalishaji wa kopa ,mwezi January mwaka huu alipata ushindi mwembamba kuchukua nafasi ya raisi Michael Sata,aliyekufa akiwa madarakani mwezi October mwaka wa jana akiwa na umri wa miaka sabini na saba wakati akipata matibabu mjini London.

Raisi Lungu ana historia ya utumbo wake wa chakula kusinyaa ambao ulifanyiwa marekebisho miaka thelathini iliyopita na ulionekana kupona lakini hali imerejea tena.

Haijafahamika mapema kama Raisi Lungu atakwenda ng’ambo kwa matibabu ,ama hata ni nchi gani atakayokwenda kupatiwa matibabu.