Putin akiri kunyakua Crimea kutoka Ukraine.

Image caption Rais wa Urusi Vladimir Putin, kwa mara ya kwanza amekiri kuamrisha unyakuzi wa jimbo la Krimea kutoka Ukraine.

Rais wa Urusi, Vladimir Putin, kwa mara ya kwanza amekiri kuamrisha unyakuzi wa jimbo la Crimea kutoka Ukraine.

Anasema hatua hiyo ilifanyika majuma kadhaa kabla ya wanajeshi wa kuruka kwa miavuli kuchukua utawala huko.

Katika hatua ya kujiandaa kutizama makala maalum ya mkanda wa video katika runinga ya taifa uitwao "Homeward Bound".

Bwana Putin, anabaini namna alivyoamrisha wakuu wa idara yake ya Ulinzi "kuanza kazi ya kuirejesha tena jimbo la Crimea kwa Urusi.".

Haki miliki ya picha
Image caption Niliamrisha vyombo ya usalama kuchukua udhibiti wa Crimea

Siku kadhaa baada ya amri hiyo kutolewa mwezi Februari mwaka jana, askari wasiojulikana walichukua udhibiti wa Bunge la Crimea na wadogo wake wakaharakisha kupiga kura ya uundwaji wa serikali mpya .

Jimbo la Crimea zamani lilikuwa sehemu lililomeguliwa kutoka Moscow tarehe kumi na nane mwezi March, na kuibua lawama kubwa Duniani.

''Moscow ilisizitiza kuwa ni raia tu wa huko ndio waliofaa kuhusishwa tu na mabadiliko hayo, licha ya kuongezeka kwa ushahidi wa wazi wa kuhusika kwa Urusi''