Mtoto anusurika baada ya kutumbukia mtoni

Image caption Mtoto wa kike alipatikana hai zaidi ya saa 14 baada ya garli alimokuwa kutumbukia ndani ya mto uliofurika huko Utah marekani

Je ushaskia kuwa watoto ni malaika ?

Amini usiamini mtoto wa kike alipatikana hai zaidi ya saa 14 baada ya garli alimokuwa kutumbukia ndani ya mto uliofurika huko Utah marekani.

Kitoto hicho chenye umri wa mwaka mmoja u nusu kilipatikana na wavuvi kinaning'inia ndani ya gari hilo lililokuwa limepinduka ndani ya mto.

Polisi wanasema kuwa mtoto huyo alipatikana akiwa ndani ya kiti cha watoto .

Alikimbizwa hospitalini katika mji wa Salt Lake City, ambapo hali yake inasemekana kuwa imeimarika maradufu.

Mamake mtoto huyo Lynn Groesbeck mwenye umri wa miaka 25 alipatikana ameaga dunia katika kiti cha dereva.

wachunguzi wanasema kuwa mamake mtoto huyo huenda aligonga vizuizi vya barabrani na kutumbukia ndani ya mto Spanish Fork usiku wa kuamkia jumamosi.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Askari watatu na zimamoto wanne walioingia ndani ya maji hayo baridi walilazimika kutibiwa hospitalini baada ya mwili wao kuganda

Mvuvi mmoja aliwaarifu polisi baada ya kuona kitoto kikielea ndani ya gari lililopinduka .

Askari watatu na zimamoto wanne walioingia ndani ya maji hayo baridi walilazimika kutibiwa hospitalini baada ya mwili wao kuganda katika operesheni hiyo.