Mgomo wa pikipiki waitikisa Chad

Image caption Biashara piki piki yazua kizaa zaa Chad

Mamlaka nchini Chadi wamechukua maamuzi magumu ya kufunga shule zote na vyuo nchini humo baada ya kutokea mgomo mkubwa wa waendesha pikipiki wanaogomea sheria mpya zinazowataka kuvaa kofia ngumu pindi wawapo kwenye shughuli zao.

Kufuatia mgomo huo watu watatu wamekwisha fariki dunia mgomo ambao unaongozwa na wafunzi kwa siku kadhaa sasa.

Usafiri wa pikipiki ni maarufu sana nchini Chad,na mar azote hutumika kama taxi na kudhoofisha biashara ya taxi na sasa wametatamua nguvu zao dhidi ya mamlaka za Chad.

Abiria nao wamepinga sheria mpya za usalama,wakidai kwamba kofia hizo ngumu ni ghali,na zinatia joto pindi mteja azivaapo kwa muujibu wa hali ya hewa.

Bei za kofia ngumu nchini Chadi imeongezwa mara dufu mara baada tu ya kutangazwa kwa sheria mpya za usalama mapema mwezi huu.