Raisi Edgar Lungu kutibiwa Afrika Kusini

Image caption Raisi wa Zambia Edgar Lungu

Raisi wa Zambia Edgar Lungu, mapema wiki hii ameelekea nchini Afrika Kusini kupata matibabu baada ya kuzimia wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mwishoni mwa wiki iliyopita .

Mapema wiki hii,Raisi Edgar Lungu alizungumza na waandishi habari kuwa kwa sasa anajisikia vizuri nah ii haizuii madaktari kufanya kazi yao,hivyo madaktari wanaosubiri kumtibia nchini Afrika Kusini wao wataamua namna ya kumtibu.

Wakati wa mkutano huo, aliwafanyia mashara waandishi habari na kuwaambia anataka kurejea Zambia akiwa hai na si mfu,na kuongeza kwamba NANI ANATAKA KUFA?

Ikumbukwe kwamba Raisi Lungu alikuwa akitoa hotuba katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mara akazimia.maafisa wa serikali nchini humo walisema kwamba kiongozi huyo mwenye miaka hamsini na nane alikuwa na malaria na uchovu mwingi.

Lakini maafisa hao hao baadaye wakaibuka na taarifa kuwa Raisi Lungu alizimia kutokana na sukari kushuka kwa kiasi kikubwa mwilini mwake .

Mtangulizi wa Raisi Edgar Lungu,marehemu Michael Sata,alifariki dumia mwaka wa jana kwa maradhi.Raisi Edgar Lungu alichaguliwa kuwa raisi wa nchi hiyo mwezi January kutumikia muda alioubakisha mtangulizi wake mpaka kufikia mwaka ujao.