Wafaransa 4 waaga Argentina

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, ameelezea masikitiko yake baada ya vifo vya watu wanane wengi wao raia wa Ufaransa.

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, ameelezea masikitiko yake baada ya vifo vya watu wanane wengi wao raia wa Ufaransa.

Wanne hao wanajumuisha pia wachezaji watatu wasifika nchini humo, walioaga dunia baada ya ndege mbili za Helikopta kugongana angani nchini Argentina.

Wakuu wametaja nyota hao kama bingwa wa nishani ya dhahabu katika uogeleaji kwenye mashindano ya Olimpiki, Camille Muffat, mwanandondi Alexis Vastine, na Florence Arthaud, gwiji katika mchezo wa upigaji makasia.

Ajali hiyo ya helikopta imetokea katika eneo lisiloweza kufikiwa kwa urahisi walipokua wakichukua picha za filamu.

Wanamichezo nchini Ufaransa wameungana kutoa rambirambi zao kwa jamaa na marafiki na haswa ulimwengu wa mechezo nchini humo kufuatia vifo vya nyota hao katika ajali hiyo mbaya.

Marubani wote wawili raia wa Argentina walifariki pia katika ajali hiyo.

Vyombo vya usalama zinasema kuwa watu 10 waliangamia katika ajali hiyo.

Walikua wakirekodi picha za filamu maarufu ya "Dropped" inayoonyeshwa kwenye Televisheni ya Ufaransa, TF1.