Mlipuko watokea kambi ya Polisi Misri

Mtu mmoja ameuawa na wengine 24 wamejeruhiwa baada ya Mtu mmoja kujitoa muhanga akilenga Kambi ya Polisi, Maafisa wameeleza.

Shambulio hilo limetokea jumanne asubuhi karibu na mji wa al-Arish.

Tukio hilo limekuja kabla ya Mkutano mkubwa wa uwekezeji unaotarajiwa kufanyika mjini humo.

Misri imekuwa kwenye vita vikubwa dhidi ya Ugaidi katika eneo la Sinai, ambao ulizidi kushika kasi tangu baada ya kuangushwa kwa utawala wa Morsi mwaka 2013.

Kundi lililokuwa likiitwa Ansar Beit al-Maqdis (washindi wa Jerusalem) lilikuwa likishutumiwa kujihusisha na mashambulizi yaliyokuwa yakitekelezwa awali.

Hata hivyo hakuna kundi lolote lililokiri kuhusika na shambulio la jumanne.

Afisa wa Polisi ameliambia shirika la habari la Ufaransa, AFP kuwa mtu huyo aliliendesha gari la kubeba maji lililokuwa na milipuko kisha aliliendesha mpaka kwenye lango la kambi ambapo Polisi walilifyatulia risasi na kusababisha gari kulipuka.