Wateja wa Safaricom na Vodacom kunufaika

Image caption Safaricom mpakani.

Mamilioni ya wateja wanaotumia huduma za M-Pesa katika nchi za Tanzania na Kenya sasa wanaweza kutuma na kupokea pesa kufuatia ushirikiano wa kibiashara kati ya waendesha huduma kwa njia ya mtandao.

Zaidi ya wateja milioni saba wanaotumia huduma za M-Pesa kwa upande wa Tanzania na zaidi ya wateja milioni 18 wanatumia hudumaya Safaricom kwa upande wa Kenya watafaidika na huduma hizo.

Mapinduzi hayo ya huduma yataruhusu huduma ya simu yenye kauli mbiu pochi kwa pochi kuhamisha fedha kati ya makampuni hayo makubwa ya huduma za simu za mkononi Afrika Mashariki.

Wateja watakuwa na uwezo wa kuhamisha fedha katika mipaka ya nchi hizo kwa gharama ile ile ya huduma za kawaida.

Image caption Vodacom kwa upande wa Tanzania

Mkurugenzi mtendaji wa huduma za Vodacom Rene Meza,nchini Tanzania anasema kwamba huduma hiyo imekuja baada ya kutafiti changamoto wanazokabiliana nazo wateja wa makampuni hayo mawili katika kutuma na kupokea pesa sawa na jirani zetu na tumekuja na ufumbuzi ulio salama,ya uhakika na rahisi katika matumizi.

Naye afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya, Bob Collymore, anaamini kwamba wamefungua ukurasa mpya katika maendeleo ya kukua kwa biashara ya M-Pesa.

Shughuli za kuwezesha mpango huo kati ya Kenya na Tanzania itawarahisishwa wafanya biashara na wateja wengine kufanya miamala yao katika mipaka ya nchi mbili hizi na itatoa fursa ya nguvu ya kubadilishana miamala kwa mara ya kwanza na malipo ya mipakani .

Takwimu zinaonesha kwamba zaidi ya pesa za Tanzania bilioni miambili huingia nchini Kenya kwa mwaka zikitokea Tanzania,wakati zinazoingia Tanzania ni shilingi bilioni ishirini na sita.