Adai mateso yamlazimisha kukiri mauaji

Haki miliki ya picha AP
Image caption Boris Nemtsov mwanasiasa wa upinzani aliyeuawa nchini Urusi hivi karibuni.

Mtuhumiwa mkuu wa mauaji ya mwanasiasa wa upinzani nchini Urusi, Boris Nemtsov amesema aliteswa ili kukiri kuhusika na mauaji ya mwanasiasa huyo.

Zaur Dadayev alishitakiwa mwishoni mwa wiki pamoja na mtu mwingine na sasa anasisitiza kuwa hana hatia.

Bwana Dadayev aliwaambia wanaotembelea magereza kwamba alifungwa kwa siku mbili akiwa ametwishwa begi kichwani na alikiri kumuua Boris Nemtsov ili rafiki yake aliyekamatwa pamopja naye aweze kuachiliwa.

Amesema amepanga kusema ukweli mahakamani, lakini hakuruhusiwa kusema.

Mtuhumiwa mwingine, Shagid Gubashev anasema alipigwa kabla ya kupelekwa Moscow.

Ameendelea kudai kuwa hana hatia. Pia watuhumiwa wengine wanne wako mahabusu.