Pakistan yavamia makao makuu ya Upinzani

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wanajeshi wa angani wa Pakistan wametekeleza msako na shambulio lisilo la kawaida katika makao makuu ya chama kikuu mjini Karachi MQM

Wanajeshi wa angani wa Pakistan wametekeleza msako na shambulio lisilo la kawaida katika makao makuu ya chama kikuu mjini Karachi MQM, na pia katika matawi ya afisi hiyo yaliyoko katikati mwa mji huo.

Maafisa wa serikali wanasema kuwa shehena za silaha zimenaswa katika afisi hizo.

Awali Mkuu wa shirila la umoja wa wa mataifa linahudumia wakimbizi wa kipalestina Pierre Krähenbühl, amelalamikia hali ilivyo katika kambi ya Yarmopuk iliyo nje ya mji mkuu wa Syria Damascus.

Anasema kuwa maelfu ya watu wanakabiliwa na hali ngumu ikiwemo ya ukosefu wa umeme, chakula na madawa.

Kambi hiyo ilijikuta ndani ya mapigano kati ya wanajeshi wa serikali na makundi ya upinzani.