Albino:Zaidi ya waganga 200 wakamatwa TZ

Image caption Mganga wa kienyeji nchini Tanzania

Zaidi ya waganga 200 wa kienyeji wamekamatwa nchini Tanzania katika juhudi za kusitisha mauaji ya Albino.

Maafisa wa polisi wamesema kuwa baadhi ya waliokamatwa walipatikana na ngozi za wanyama na dawa za kienyeji.

Albino pia wamepewa vifaa vya kupiga kamsa iwapo watashambuliwa.

Umoja wa mataifa unasema kuwa takriban albino wapatao 76 wameuawa nchini Tanzania tangu mwaka 2000.

Image caption Vifaa vya waganga wa kienyeji nchini Tanzania

Vipande vya miili yao hutumika na waganga wa kienyeji kwa kuwa vinaaminika kuvuta bahati .

Rais Jakaya Kikwete ameelezea mauaji hayo kama aiabu kwa taifa.