Polisi wawili wajeruhiwa mjini Ferguson

Haki miliki ya picha AP
Image caption Polisi mjini Ferguson wameshutumiwa kutenda kazi kwa ubaguzi

Maafisa Polisi wawili wameshambuliwa kwa risasi mjini Ferguson, mji ambao umekuwa katika hali ya wasiwasi mwingi tangu kijana mweusi alipouawa na askari wa kizungu mwezi Agosti.

Afisa mmoja alipigwa usoni mwingine alijeruhiwa begani.Polisi wanasema wote wanapata matibabu hospitalini.

Shuhuda wa tukio hilo ameiambia BBC kuwa aliwaona maafisa wakiwa wametapakaa damu.

Shambulio la risasi lilitokea nje ya jengo la idara ya Polisi, ambako waandamanaji kadhaa walikusanyika baada ya Mkuu wa Polisi mjini humo Thomas Jackson alipotangaza kujiuzulu.

Idara ya Polisi ilikosolewa kuwa tukio la kuuawa kwa kijana huyo lilikua na viashiria vya ubaguzi wa Rangi.

Afisa mkuu wa utawala wa eneo la Furguson na Jaji wa manispaa ya mji huo walijiuzulu mwanzoni mwa juma hili.