Kamanda wa polisi Ferguson ajiuzulu

Haki miliki ya picha AP
Image caption Polisi wa mji wa Ferguson

Kamanda wa polisi katika mji wa Ferguson nchini Marekani amejiuzulu baada ya ripoti ya shirikisho kulaumu kitengo chake kina ubaguzi.

Thomas Jackson anakabiliwa na miito ya kumtaka ajiuzulu tangu yalipotokea maafa ya kuuawa kwa kupigwa risasi kwa Michael Brown, kijana mweusi ambaye hakuwa na silaha yoyote wakati tukio hilo likitokea.

Kijana huyo aliuawa na mmoja wa maafisa wake Agusti mwaka jana.

Meya wa eneo hilo James Jackson amemuelezea kamanda huyo wa polisi kama mtu muadilifu ambaye anatumai kuwa kuondoka kwake kutasaidia jamii kumaliza machafuko yaliyofuatia baada ya mauaji hayo.

Afisa wa ngazi za juu katika utawala wa mji wa Frguson na Jaji wa manispaa walijiuzulu mapema wiki hii.