Madonna:Nawapenda vijana wadogo

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Msanii wa muziki wa Pop Madonna asema kuwa yeye huvutiwa sana na vijana wadogo badala ya wanaume wa umri wake

Msanii wa nyimbo za Pop Madonna aliyesifika kwa wimbo wake 'material girl' na ambaye amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mchezaji densi Brahim Zaibat ambaye amempita kwa miaka 28 pamoja na Timor Steffens mwenye umri wa miaka 27, amesisitiza kuwa anavutiwa na vijana wadogo kwa kuwa hawezi kuanza uhusiano na wanaume wa umri wake ambao anasema wameoa na wana watoto

Alipoulizwa ni kwa nini yeye huwapenda vijana wadogo,aliliambia gazeti la New York Daily News,kwamba wanaume wengi wa umri wake wameowa na wana watoto.

''Huwezi kuanza nao uhusiano.Mimi hupendelea kupata uzoefu na kujaribu mambo mapya.Mimi ni mama wa watoto wanne.kwa hivyo ni lazima uwe na mawazo huru na uwe mtu anayependa kujaribu mambo mapya kwa wewe kuweza kuingiliana na maisha yangu'',alisema Madonna.

''Watu wenye umri mkubwa na ambao wana mwelelekeo fulani hawapendi mambo mapya ukilinganish na vijana wadogo'',aliongezea.

Wakati huohuo msanii huyo ambaye alikuwa ameolewa na Guy Ritchie mwenye umri wa miaka 46 na Sean Penn mwenye umri wa miaka 54 hivi majuzi alikiri kwamba atafunga ndoa nyengine iwapo atampata wa kumliwaza.