Watu 3 wakamatwa wakisafirisha Miraa UK

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mfanyibiashara wa Miraa.

Maafisa wa polisi wamewakamata wanawake watatu raia wa Indonesia katika uwanja wa ndege wa Moi mjini Mombasa Kenya wakijaribu kusafirisha kilo 61 za miraa nchini Uingereza.

Miraa hiyo inadaiwa kuwa na thamani ya millioni 20 fedha za kenya katika soko la Uingereza.

Miraa hiyo ilipatikana imefungwa katika mabagi manne ikitarajiwa kusafirishwa hadi soko la Ulaya kupitia taifa la Denmark.

Afisa mkuu wa Polisi katika uwanja wa ndege wa Mombasa Richard okweya amesema watatu hao walipanda ndege ya biashara hadi uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta kabla ya kuelekea Denmark.

Polisi wamesema kuwa Tsomodis Sarina,Jepsen Jesica na Helberg Isabel waliwasili nchini Kenya wiki moja iliopita.Seriokali ya Uingereza ilipiga marufuku matumizi ya miraa nchini humo.