Wanawake wanaovaa nguo nyekundu huvutia

Image caption Mwanamke aliyevalia vazi jekundu huvutia kulingana na utafiti

Wanawake wanaovalia mavazi ya rangi nyekundu huwavutia sana wanaume ikilinganishwa na wale wanaovaa mavazi ya rangi nyengine.

Kulingana na utafiti huo rangi hiyo huvutia sana na pia huwashirikisha wanawake wanaobeba laptopu nyekundu.

Steven G Young wa chuo kikuu cha mji wa New York aliandika katika jarida la maadili ya kisosholojia: Ushahidi wa hivi karibuni unadai kwamba rangi husaidia katika kuwakutanisha watu wawili wanaopendana kwa kuwa raha inayopatikana miongoni mwa wanawake wakati wa tendo la ngono hushirikishwa na wekundu wa mashavu,shingo na kifua.

Wanawake wengi hupendelea kuvaa mavazi ya rangi nyekundu wakati wanapojiandaa kukutana na wanaume wanaowavutia.

Ukilinganisha na rangi nyengine wanawake wanaovalia mavazi ya rangi nyekundu huvutia sana.