AI:Walemavu wako hatarini Somalia

Image caption Walemavu nchini Somalia

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International linasema kuwa watu wenye ulemavu wa kimwili nchini Somalia wako kwenye hatari kubwa ya kushambuliwa , kubakwa na kuondolewa kwa lazima makwao.

Ripoti mpya inasema kuwa mzozo wa zaidi ya miongo miwili nchini humo umewaacha watu walemavu katika hali mbaya.

Amnesty imeitaka serikali ya Somalia kufanya jitihada zaidi za kuwalinda watu hao.