Al-Shabaab:Gavana anusurika kifo Kenya

Image caption Gavana Ali Roba wa kaunti ya Mandera

Mwanasiasa mmoja wa Kenya amenusurika shambulizi lililotekelezwa na kundi la Al shabaab.

Ali Roba ,ambaye ni gavana wa mji ulio mpakani wa Mandera alikuwa akisafiri kuelekea mjini humo wakati msafara wake ulipovamiwa.

Jaribio hilo sio la kwanza kuhusu maisha ya mwanasiasa huyo ambaye amekuwa akiongoza kampeni dhidi ya kundi hilo katika eneo hilo.

Wapiganaji hao tayari wamekiri kutekeleza shambulizi hilo na kusema wamefanikiwa kuwaua wanajeshi wanne,kuchoma magari mawili na kutoroka na jengine.

Kufikia sasa polisi wa Kenya hawajathibitisha matamshi hayo ya kundi hilo.

Image caption Al shabaab

Tukio hilo lilitokea katika barabara ambapo watu 28 waliokuwa wakisafiri katika basi walivamiwa na kuuawa miezi minne iliopita.

Barabara hiyo iko karibu na mpaka na Somali.