K Kazkazini yarusha makombora baharani

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Meli ya kijeshi ya Korea kazkazini yarusha makombora Baharini

Wizara ya ulinzi nchini Korea Kusini inasema kuwa Korea Kaskazini imefyatua makombora mawili ya masafa marefu kwenda baharini eneo la pwani ya mashariki.

Kisa hicho kinaripotiwa wakati kukiwa na msukosuko katika rasi hiyo huku korea kusini na marekani wakiendelea mazoezi ya kijeshi ya kila mwaka.

Korea na marekani wanaseme kuwa mazoezi hayo ni ya kujlinda lakini korea kaskazini inayaona kuwa ya kutaka kuivamia.