Upandikizaji wa uume wafaulu Afrika Kusini

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Upandikishaji wa uume wafanikiwa Afrika kusini

Kundi la madaktari wa upasuaji kutoka Afrika kusini limefanikiwa upandikizaji wa uume wa mwanadamu.

Oparesheni hiyo iliochukua masaa manane ilifanywa mnamo mwezi Disemba katika hospitali ya Tygerberg mjini Cape Town kupitia ushirikiano wa chuo kikuu cha Stellenbosch.

Inadaiwa kuwa jaribio la pili la upasuaji huo kufanywa.

Madaktari wanasema kuwa mgonjwa aliyefanyiwa upandikishaji huo amepona.

Uume wake ulikatwa baada ya matatizo yaliosababishwa na kupashwa tohara.