Rufaa ya Oscar Pistorious yatupwa

Image caption Oscar pistorius akiwa mahakamani

Mawakili wa mwanariadha mlemavu wa Afrika kusini Oscar Pistorius anayehudumia kifungo jela wamepoteza kesi ya rufaa kuhusu hatua ya mahakama ya kumuondolea mashtaka ya mauaji.

Jaji Thokozile Masipa ametoa uamuzi katika mahakama ya Johannesburg kwamba ombi hilo likataliwe.

Pistoris alimpiga risasi na kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp mnamo mwezi Februari 2013.

Alipewa hukumu ya miaka 5 jela kwa mashtaka ya mauaji ya kutokusudia.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Oscar Pistorious

Baada ya kusikizwa kwa rufaa hiyo ,jaji Masipa alisema kuwa maelezo hayamruhusu kusikiza ombi hilo ama hata kulitupilia mbali.

''Maoni yangu ni kwamba iwapo nitaliruhusu ombi hilo nitakuwa nauangazia upya uamuzi wangu'',alisema Masipa.

Mwanariadha huyo aliye na ulemavu wa miguu yote miwili aliondolewa mashtaka yote mawili ya mauaji ya kukusudia.