Unene wamfanya kukosa burudani Uingereza

Haki miliki ya picha AFP
Image caption klabu ya burudani nchini Uingereza

Mama mmoja amedai kuwa yeye na marafiki zake wawili walizuiliwa kuingia katika kilabu moja ya burudani kwa sababu zinazodaiwa kuwa ni wanene sana na wenye sura mbaya

Stacey Owen 33, alikuwa ametoka na marafiki zake wawili kwa ajili ya kupata burudani wakati wa usiku siku ya jumamosi alipokataliwa kuingia katika baa moja jijini Manchester kwa sababu ya unene wake.

Stacey amesema wao walizuiwa huku watu wengine wakiingia katika baa hiyo maarufu mjini humo,

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Klabu ya burudani Uingereza

Mama huyo sasa anataka kuombwa radhi na wamiliki wa Baa hiyo lakini mpaka sasa amedai hajapata ujumbe wowote kutoka kwao.

Anasema sio kwamba anajiona kwamba yeye ni mrembo sana lakini kilichomshangaza ni uwepo wa ubaguzi huo miongoni mwa wateja.