Washtakiwa kwa kutaka kujiunga na IS

Image caption washtakiwa kwa kutaka kujiunga na IS

Watu watatu wenyeji wa mji wa New York nchini Marekani wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashtaka ya kujaribu kuwasaidia wanamgambo wa Islamic State.

Watatu hao amabao wote ni raia wa mataifa ya Asia walikamatwa mwezi uliopita baada ya mmoja wao kutoka nchini Kazakhstan alipojaribu kuabiri ndege kuenda nchini Uturuki akiwa na mpango wa kujiuga na wanamgambo la Islamic State.

Wote hao walikana mashtaka hayo.

Kesi yao itasikilizwa tena tarehe 19 mwezi juni.