Hali ya hatari yatangazwa Vanuatu

Haki miliki ya picha AP
Image caption Hali ilivyo kisiwani Vanuatu

Rais wa Vanuatu ameiambia BBC kuwa watu wengi nchini humo wameachwa bila makao kutokana na kimbunga kikali kilichokumba kisiwa hicho cha pacific siku ya ijumaa.

Akizungumza kutoka nchini Japan ambapo amekuwa akihudhuria mkutano wa umoja wa mataifa, alisema kuwa majengo mengi kwenye mji mkuu zikiwemo shule na ya vituo vya afya yameharibiwa na kimbunga pam.

Utawala nchini humo umetangaza hali ya hatari,huku mawasiliano yakiwa hayapo karibu kote kisiwani humo, hakuna habari kuhusu hali ilivyo kwenye visiwa vingine ambavyo ni makao kwa karibu watu 90,000

Haki miliki ya picha AP
Image caption Hali ilivyo kisiwani Vanuatu

Msaada wa kwanza tayari umewasili kutoka nchini New Zealand huku Australia nayo ikitangaza kutoa msaada pamoja na Uingereza na umoja wa mataifa.