Mabomu mtawanyiko yatumiwa Libya

Mabomu mtawanyiko Haki miliki ya picha BBC World Service

Shirika la kimataifa la kutetea haki za kibinaadamu lenye makao yake New York linasema kuna ushahidi wa kuaminika kuwa mabomu mtawanyiko yametumiwa katika mapigano ya karibuni nchini Libya.

Human Rights Watch inasema mahojiano iliyofanya kwa simu na ushahidi wa picha unadhihirisha kuwa mabomu hayo yalirushwa katika maeneo ya Sirte na Bin Jawad, katikati ya nchi.

Jeshi la serikali ya Libya inayotambuliwa kimataifa inaripotiwa limekiri kuwa lilishambulia maeneo hayo, lakini linakanusha kuwa lilitumia mabomu mtawanyiko.

Mabomu hayo ambayo yanatawanya mabomu madogo-madogo katika eneo kubwa, yamepigwa marufuku na nchi nyingi kwa sababu yanaumiza watu ambao sio waliolengwa.