Milipuko yalenga makanisa Pakistan

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wasichana walia kufuatia mashambulizi mawili yaliolenga makanisa Pakistan

Mabomu mawili yamelipuka yakilenga makanisa mawili yaliyokuwa yamejaa watu kwenye mji wa Lahore chini Pakistan wakati watu walipokuwa wakihudhuria misa ya jumapili.

Polisi wanasema kuwa takriban watu 6 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Mashambulizi hayo yanaoyoaminika kuwa ya kujitoa mhanga yalifanyika eneo lenye waumini wengi wa kikristo la Youhanabad

Sehemu ya kundi la Taliban linalofahamika kama Jamatul Ahra limesema kuwa ndilo lililoendesha shambulizi hilo.