Waliotaka kujiunga na IS wakamatwa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wapiganaji wa islamic state

Polisi mjini London wanasema kuwa vijana watatu wa Uingereza wamekamatwa nchini Uturuki wakiwa safarini kuelekea nchini Syria ili kujiunga na wapiganaji wa Islamic State.

Watatu hao kutoka London akiwemo kijana wa miaka 19 na vijana wengine wawili wenye umri wa miaka 17 walikamatwa siku ya ijumaa baada ya maafisa wa polisi nchini Uingereza kuiarifu serikali ya Uturuki.

Mnamo mwezi Februari ,wasichana watatu kutoka Uingereza walisafiri kutoka mjini London kuelekea Uturuki wakiwa na lengo la Kujiunga na wapiganaji wa IS.

Kwa sasa wasichana hao wanadaiwa kuwa nchini Syria .