Shambulizi laua 45 Nigeria

Image caption Wanawake na watoto wachanga zaidi ya 45 wameuawa katika shambulizi lililotekelezwa katika kijiji kimoja huko Egba katika jimbo la Benue Nigeria

Wanawake na watoto wachanga zaidi ya 45 wameuawa katika shambulizi lililotekelezwa katika kijiji kimoja huko Egba katika jimbo la Benue Nigeria.

Maafisa wa usalama katika jimbo hilo la kati wanasema kuwa wavamizi walishambulia kijiji hicho alfajiri kuamkia leo .

Hata hivyo,mwanasiasa mmoja kutoka eneo hilo Audu Sule ameiambia BBC kuwa zaidi ya watu 81wamauawa na watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki aina ya Kalashnikov.

Awali mapigano kati ya jamii ya wafugaji wa kuhama hama ya Wafulani na jamii za wakulima yamekuwa yakisababisha maafa makubwa.

"Walianza kufyatua risasi kiholela wakati kijiji kizima kilikuwa kimelala waliouawa wengi ni wanawake na watoto wachanga," alisema bwana Sule .

Image caption Asilimia kubwa ya waliouawa ni kinamama na watoto

Polisi wameanza msako kubaini ni kina nani waliotekeleza shambulizi hilo.

Msemaji wa polisi Austin Ezeani ameliambia shirika la habari la AFP kuwa eneo hilo limekuwa likikumbwa na mapigano ya kila mara .

Maafisa hawajabaini iwapo ilikuwa shambulizi la kigaidi au ilikuwa ni shambulizi baina ya jamii hasimu zinazoishi katika jimbo hilo la Benue

Mwakauliopita mvutano kuhusu maeneo ya kulisha ng'ombe yalisababisha mauaji ya wanavijiji 100 katika jimbo la kati la Kaduna.