Huwezi kusikiliza tena

DRC kukata mbuga ya Virunga kuruhusu uchimbaji madini

Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo inasema kuwa inataka kuchora upya mpaka wa Mbunga kubwa ya kitaifa ya wanyama Pori ya Virunga, na ambayo pia ni eneo la dunia la lihistoria, ili kuruhusu shughuli za uchimbaji mafuta.

Waziri mkuu wa Nchi hiyo Matata Ponyo, ameiambia BBC kuwa, kuna mazungumzo yanayoendelea kati ya serikali na shirika la Unesco.

Kampuni hiyo imefanya utafiti wa upatikanaji wa mafuta katika msitu huo, wenye sokwe ambao wamo katika hatari ya kuangamia Duniani.

Hata hivyo shutuma kali kali zimetolewa kutoka kwa wana mazingira na makundi ya haki za binadamu .

Hii hapa Taarifa yake mwaandishi wa BBC Maud Jullien.