Reading kupambana na Arsenal FA

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wachezaji wa Reading wakifurahia kufuzu hatua ya nusu fainali ya kombe la FA baada ya kuichapa Bradford 3-0

Mashindano ya FA CUP yaliendelea tena usiku wa kuamkia Jumanne kwa mchezo mmoja wa hatua ya robo fainali kupigwa.

Klabu ya Reading kwa mara ya kwanza katika kipindi cha takriban miaka 88, imeweza kutinga katika hatua ya robo fainali ya kombe la FA baada ya kuibugiza Bradford mabao 3-0.

Timu hiyo sasa itavaana na mabingwa wa tetezi wa kombe hilo Arsenal kati ya April 18 au 19, katika mchezo wa nusu fainali.

Na katika ligi kuu ya England Liverpool imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Swansea City. Liverpool imecheza mchezo wa 13 bila kupoteza hata mechi moja.

Kwa matokeo hayo Liverpool imezidi kuzifukuza timu za juu katika kuwania nafasi ya nne bora. Liverpool ina pointi 54 pointi mbili nyuma ya Manchester United yenye pointi 56 katikja nafasi ya nne. Chelsea inaongoza kwa pointi 64 ikifuatiwa na Manchester City yenye pointi 58 na Arsenal iko katika nafasi ya taut ikiwa na pointi 57 pointi moja nyuma ya Manchester City.