Mwanasheria wa daktari wa Osama auawa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Samiullah Afridi,aliye uawa na Talbani

Aliyewahi kuwa mwanasheria wa Daktari wa Osama bin Laden, Samiullah Afridi ameuawa kwa kupigwa risasi huko Pakistan.

Mtu aliyekuwa na silaha alimmshambulia Samiullah Afridi ambaye alikuwa ndani ya gari lake akiendesha eneo la Peshawar.

Samiullah Afridi alikuwa mmoja wa wanasheria wa Dr.Shakeel Afridi ambaye ndiye aliyefichua siri kwa Marekani juu ya wapi alikokuwa Ossama Bin Laden ambaye alikuwa mafichoni huko Pakistani kwa takribani miaka minne.

Dr Afridi wakati anauawa alikuwa katima matembezi alifungwa kifungo cha muda mrefu.Kundi la Talbani limekiri kutekeleza mauaji hayo.