Rais Putin apuuza uvumi kuhusu afya yake

Image caption Rais Vladmir Putin wa Urusi

Rais Vladmir Putin wa Urusi amebeza uvumi kuhusu afya yake katika siku yake ya kwanza kuonekana hadharani baada ya siku kumi.

Kiongozi huyo wa Urusi amesema"maisha yangekuwa ya kuchosha iwapo kusingekuwa na umbeya", lakini ameshindwa kueleza kuhusu kutoonekana kwake hadharani kwa kipindi hicho na kufuta ratiba iliyomtaka kuhudhuria matukio kadha aliyokuwa amepangiwa.

Alionekana katika mkutano na rais mwenzake wa Krygyzstan Almazbek Atambayev katika kasri ya Constantine karibu na mji wa St Petersburg.

Bwana Putin Jumatatu alitoa amri kwa askari karibu elfu arobaini wa jeshi la wanawamaji wa Urusi kujiandaa kwa mazoezi ya kivita, hatua ambayo huenda ikawa ni kujibu mazoezi ya majeshi ya NATO yaliyofanyika karibu na nchi hiyo.