Mamilioni ya dola kurejeshwa Switzerland

Haki miliki ya picha nigeria at 50
Image caption Hayati Sani Abacha,Rais wa zamani wa Nigeria

Serikali ya Switzerland inatarajiwa kurejesha kiasi cha dola za Kimarekani milioni 340 ambazo zilikuwa zimeibwa wakati wa miaka ya 1990 wakati Rais Sani Abacha akiwa kiongozi wa Nigeria.

Baada ya Bwana Abacha kufariki dunia mwaka 1998, Nigeria iliiomba Uswiss kusaidia kupatikana kwa zaidi ya dola bilioni mbili zilizokuwa zimehifadhiwa katika mabenki ya Ulaya na wana familia wa Rais Abacha.

Uswiss mwaka uliopita ilirejesha dola milioni mia saba kwa serikali ya Nigeria baada ya kumaliza mvutano wa kisheria.

Rushwa inabaki kuwa tatizo kubwa nchini Nigeria na katika mataifa ya nchi nyingi zinazoendelea hususan kutoka Afrika ambako wanasiasa mbalimbali wanatuhumiwa kujilimbikizia fedha katika mabenki ya Ulaya.