Azuiliwa kusafiri Syria kujiunga na IS

Haki miliki ya picha Facebook
Image caption Brian de Mulder mmoja wa vijana waliojiunga na kundi la islamic state kutoka ubelgiji

Mvulana mwenye umri wa miaka 16 nchini Uingereza amepigwa marufuku kusafiri nje ya nchi hiyo kutokana na hofu kwamba huenda akaenda kupigana kama mwanajihadi Syria.

Kakazake wakubwa wawili wameuawa wakipigana katika kundi la Nusra Front -- kundi la waasi wenye itikadi kali za kiislamu linalohusishwa na Al Qaeda.

Jaji mmoja London, alitoa agizo hilo la mahakama kutokana na ombi la maafisa wa serikali waliosema wanataka kumlinda asiuawe.

Jaji huyo alieleza mahakama kwamba wanaume wa familia ya kijana huyo ambao wanatoka Libya, wamejihusisha kikamilifu kupigana jihad Syria, na mamake amechoshwa kwa huzuni.